HOME.

Wilaya ya Lushoto ilianza kabla ya Uhuru wa Tanganyika. Chini ya utawala wa kikoloni ambapo ilijulikana kama Usambara. Jina la Lushoto lilitungwa/kuandikwa na Mzungu aliyewauliza wenyeji jina la eneo zima akaambiwa ni Lushoto wakimaanisha kichaka cha kujificha. Mzungu akaliandika kwenye daftari lake na akaliweka kwenye ramani kuwa eneo hilo ni Lushoto kwa kujua ndilo jina la eneo. Hivyo jina la Usambara likapotea na kubakia jina la Lushoto. Eneo la Lushoto kabla na baada ya Uhuru mpaka 1966 lilikuwa linajumuisha eneo la Wilaya ya Korogwe. Wilaya ina eneo lenye kilomita za mraba 3,500 zenye Tarafa 8, Kata 44, vijiji 207 na vitongoji 1,669 zenye kadirio la watu 507,302 kwa mwaka 2012. Mkuu wa Wilaya wa kwanza alikuwa Mhe. Rajabu Semvua na Afisa wa Wilaya ndiye aliyekuwa akifanya kazi ya Hakimu wa Wilaya. Hata hivyo utawala wa mazumbe pia uliendelea mpaka baada ya Uhuru. Wilaya hii iko kwenye Milima ya Usambara na wakazi wake wanajishughulisha na kilimo cha matunda na mboga mboga kwenye mabonde yanayopatikana kwenye Wilaya.